Namna ya Kuhesabu Mzunguko Wako Wa Hedhi

​​Angalia mfano huuu

Asha wa Makolola Tanga

Amepata bleed tarehe 01/03/2017 alafu akaendelea kutoka damu tarehe tarehe 02, tarehe 03, tarehe04 tarehe 05
Kisha akaja kupata tena bleed tarehe 29/03 na akaendelea hadi tarehe 04/04
 SASA

Asha siku yake ya kwanza ya mzunguko wake wa hedhi wa mwezi wa 3 ni tarehe01

Siku yake ya mwisho ya mzunguko wa hedhi wa mwezi wa tatu ni tarehe 28/03 sio 29/03

Asha anamuznguko wa siku 28 – yaani ukihesabu siku kuanzia tarehe moja hadi tarehe 28 unapata siku 28
Siku za hedhi au siku za bleed mwezi wa tatu ni kuanzia tarehe 01/03 hadi tarehe 05 mwezi wa 3

Siku za bleed za asha ni 5 kuanzia tarehe 01 hadi tarehe 5
Ni muhimu sana kujua mambo haya kabla hujaanza kuliza maswali mengine
Ikiwa Asha atapata tena bleed ingine mwezi wa nne tarehe26 basi asha atakwa tena na mzunguko wa hedhi wa siku 28 kwa mwezi wa nne
yaani kuanzia tarehe 29/03 hadi tarehe 25/04.

Yaani atahesabu hivi

tarehe 29/03 siku ya kwanza ya mzunguko

tarehe 30/03 siku ya pili ya mzunmguko

tarehe 31/03 siku ya tatu ya mzunguko

tarehe 01/04 siku ya nne ya mzunguko
hadi afike tarehe 25

tarehe 26 amepta bleed – tarehe 26/04 itakuwa siku ya kwanza ya mzunguko mwingine
ANGALIZO

 hapo, akipata bleed tarehe 10 basi mzunguko uliopita unaishia tarehe 09, na mwingine unaanza tarehe 10 >>> usichanganye
ikiwa Asha alikuja pata tena bleed yake ingine tarehe 24/05 basi kwa mwezi wa tano Asha alikuwa na mzunguko tena wa siku 28 yaan hesabu siku kuanzia siku ya tarehe 26 mwezi wa 4 hadi tarehe 23 mwezi wa tano utapata siku 28
 Kwa hiyo tarehe za saha za bleed za miezi mitatu ni

01/03/2017

29/03/2017

26/04/2017

24/05/2017

Na hapa ndio swali huwa linajitokeza

Mwalimu mbona mimi tarehe za hedh zinarudi kwa nyuma, zinapungua siku 2  mbili? Sasa mimi kama mwalimu najua iko shida na huyu mtu kubwa sana namwambia nipigie jioni – sasa yeye anadhani laabda sijui au nimeshindwa hapigi na anaingia mtini lakini kwa sababu najua akili zetu waswahili nampigia bada ya dk 3 nakata simu ili apige nimpe maelezo vizuri
Kwa hiyo kwa bahati nzuri Asha wetu ni mwanamake mwenye bahati na anamzunguko wa siku 28 na kwa hiyo kazi kwetu ni rahis sana – kumbuka mfano wa Asha n i kwa ajili ya siku 28 tu lakini sio wote wenye mzunguko wa siku 28 kwa hiyo usikariri- na zile namba kwenye gurudumu sio tarehe ni siku za hedhi, yaani siku ya kwanza, ya pili , ya tatu hadi siku ya 28
 mfano mt amepta bleed tarehe 15/06 basi siku yake ya kwanza ya mzunguko wa hedhi ni tarehe 15/06

ndio inaanza pale kwenye 01 kwenye gurudumu
Sasa tuje kwenye siku za hatari, salama na za uzazi.
Kumbuka mambo makuu yafuatayo

– siku ya mimba ni moja tu

– yai likishatoka kwenye mji wa mayai huishi masaa24 tu

– mbegu za kiume zikishaingia ukeni huishi ndani ya mwanamke kwa siku 3 tu yaani masaa72

– unaweza pata mimba wakati uko bleed
 Mwanamke akipata bleed haimaanishi yai limepasuka, bali ni kuwa mji wa mimba umevunja nanga au umebomoa nyumba ya kupokelea kijusi (mtoto wa siku kadhaa) yaani mji wa mimba hujiandaa kupokea mimba kwa kujenga kuta za mji wa mimba kwa damu – so mimba isipokuwepo basi ule ukuta unabomoka
kubomoka miji wa mimba ndio kujianda kujenga mji mwingine kwa ajili ya yai lingine la mwezi mwingine

kwa hiyo mwanamke akipata bleed tu tayari mwili unaanza maandalizi ya kupokea mimba ingine – ki2 hiki hufanyika kila mwezi
Sasa ugunduzi wa kisayansi na wa uhakikia unasema ya kwaamba kutoka siku ya bleed umeanza kurudi nyuma hadi siku yai lilitoka basi ni siku 15 (siku ya yai kutoka ndio siku ya kupata mimba) siku ya kupata mimba tumesema ni moja tu
 Sasa ugunduzi wa kisayansi na wa uhakikia unasema ya kwaamba kutoka siku ya bleed umeanza kurudi nyuma hadi siku yai lilitoka basi ni siku 15

👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿
mfano tunaweza jua siku ile moja ya asha kupata mimba kila mwezi

29/03/2017

hesabu siku 15 ktoka tarehe 29 na kurudi nyuma

29/03 ya kwanza

28/03 ya pili

27/03 ya tatu

26/03 ya nne

nakuendelea
 Njia rahisi ni kuchukua mzunguko wake na kutoa na 14
au kama una kalenda ni rahisi zaidi
 kwa hiyo kwa mwezi wa tatu asha siku yake ya kupata mimba ni siku ya 14 yaani 28-14 = 14

mwezi wa nne itakuwa hivyo hivyo nakadhalika

Lakini sasa unatakiwa ujue siku ya 14 ni tarehe ngapi

mwezi wa 3 itakuwa tarehe 14/03

mwezi wa nne itakuwa tarehe 12/04

mwezi wa tano itakuwa tarehe 08/05
sasa unakumbuka ya kwamba kama angekuwa ng’ombe basi tarehe 14 ndio unampelekea kwa dume – anashika mimba shap bla ubishi
Lakini huyu ni binadamu – ndio mana mbegu za kiume huishi siku 3+
kwa hiyo asha hata kama atafanya mapenzi siku 3 kabla ya tarehe 14 bado anaweza pata mimba, kzo m,begu zitaingia na kukaa zikisubiria yai litoke tarehe 14
HAPO TUKO PAMOJA??
KWA hiyo siku za uzazi – yaani siku ambazo ni most likely yaani ni rahis sana kupata mimba ni siku 3-4 kabla ya siku ya kupata mimba na kwa mfano huu ni siku ya 14,13,12,11,10
KWA hiyo siku za uzazi – yaani siku ambazo ni most likely yaani ni rahis sana kupata mimba ni siku 3-4 kabla ya siku ya kupata mimba na kwa mfano huu ni siku ya 14,13,12,11,10
Sasa mwili wa asha sio machine – unaweza chenji muda wowote lakini kubadilika kwake haiwez kuwa kubwa sana, kwa hiyo ili kupata siku za hatari siku ambazo kuna uwezekano wa kupata mimba angalua siku 3-4 huongezwa tena mbele ya siku ya 14
 ndio unapata siku ya 11-18 kwa mzunguko wa siku 28
Sasa kwa mfano huu, ukisikia nasema ziku za uzazi namanisha zile siku 4, yaani siku ya mimba na siku 3 kabla

na nikisema siku za hatari namaanisha siku zote kuanzia siku ya 11-18

 ANGALIA TOFATI

kama mtu anatafuta mimba basi atasuata siku za uzazi yaani zile siku 4

kama mtu hataki mimba basi bora asifanye tendo la ndoa siku zote 11-18. kwa kuwa siku yeyote hapo unaweza pata mimba hata kama sio siku ya uzazi kutokana na mabadiliko mbalimbali niliyokwwisha yasema
 Kwa kanuni hii – mzunguko wowote unaoenda kwa siku kamili kila mwezi au tofauti kidogo na hapo basi utatumia kanunu hii hii – na sio tofauti na hapo.

Maoni Na Ushauri

Mawasiliano 

Call/Sms/Whatsapp +255714206306

Mail: khalidgugu@gmail.com

Fb page: Afya Ya Uzazi Na Ushauri 

Blog: khalid1710.wordpress.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s