Dondoo za Kuzingatia Kabla,  Wakati Baada Ya ujauzito 

​ Habari za jioni. 

Leo tunaendelea na mada yetu ya yakuzingatia kabla,  wakati na baada ya ujauzito.

Mara nyingi,  Week ya 30 mtoto hugeuka na hivyo kichwa kuelekea usawa wa njia ta kutokea. Wengi hupata maumivu Kama ya uchungu na baadhi wanaweza ona damy nyepesi. Waswahilu tunaita pundu.  Kama maumivu yatadumu muda mrefu ni vyema mama akawahi kituo cha afya. 

Je mama atajuaje dalili za kujifungua. Mara nyingi mama atapata maumivu ya mgongo,  miguu na maumivu Kama ya tumbo la siku. Kama itafika wiki ya 36 mtoto hajageuka, mama atahitaji kuwa chini ya uangalizi wa madaktari pindi tar zake za kujifungua zitakapofika. Wengi hufanyiwa upasuaji. 

1. Katika Hatua za awali za uchungu njia huwa chini ya cm 3, hivyo mama hushauriwa kutembea,  kuoga,  kusikiliza mziki au kuangalia videi,  kunywa vimiminika Kama chai.

 Kama uchungu utadumu kwa muda mrefu bila kujifungua,  mama atatakiwa kuwa chinu ta uangaluzi na hata kuongezewa njia ikuhitajika. 

Baadhi hupata uchungu na kukata, madaktari hupima mapigo ya Mtoto baada ya muda na wanaweza pewa dawa za  kuongezewa uchungu ( zinauma balaa). 

Ikishindikaba mama atafanyiwa upasuaji kunusuru maisha ya mtoto

 Zipo njia za Kupunguza maumivu ya uchungu Kama  kutembea, mwanga hafifu,  maombi,  kusikiza mziki laini. 

Pia wengine hujifungua katika maji maalum,  kukaa juu ya mpira wa kujifungulia,   kuchua taratibu mgongo,  tumbo na miguu kwa kutumia mafuta ya nazi nk

 Pia ni vyema wauguzi wakaangalua presha ta mama na sukari kila mara kwa mama mwenye uchungu wa muda mrefu,  wengine wanaweza kuishiwa nguvu na kuzimia au kupata kifafa na hivyo kugatarisha maisha ya mtoto

Nimeshuhudia manesi wakimwambia mama mmoja akishajifungua ndio awaite. 

🌚🌚. 

Akizimia je

Baadhi ya Hospital zetu ni changamoto jamani haswa za wa mama

Wamama wengi huishiwa nguvu mapema sababu hutumua nguvu nyingi kusukuma mtoto,  ila tafiti zimeonesha Kama njia itafunguka hadi cm 10 mtoto hushuka mwenyewe kwa kujisukuma, hivyo jitihada ya mama uhitajika kidogo tu kumuwahisha mtoto duniani.

Kwa mama aliyeongezewa njia au kuchanika msamva atashonwa njia (mara nyingi hamna ganzi) na baada ya muda maumbile yake yatarudi kawaida tofauti na baadhi ta wamama wanavyo hofu

 Kwa mama aliyefanyiwa upasuaji ni vyema akapumzika baada ya kuamka la sivyo wengi hipata maumuvu makali ya kichwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s