Dondoo Baada Ya Kujifungua 

​Habari,  tunaendelea na somo letu. 

Tafiti zinaonesha ni vyema kusubiri takribani sekunde 60 baada ya mama kujifungua,  ndio kitovu kikatwe. 

Inasemekana zile taarifa nyingi za  kinga hutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa kutumia kitomvu

 Pia yale maziwa ya kwanza ya njano ni muhimu sana kwa mtoto,  kwani huwa na kinga kwa wingi,  pia huwa na virutubisho ambavyo ni muhimu kwa afya ya ubongo pamoja ukuaji kwa ujumla

 Kama mama maziwa hayatoki ni vyema akakulku down kama ana stress,  akanywa vimiminika vya uvuguvugu kama chai ya tangawizi,  uji wa pilipili mtama. 

Pia ampe mtoto ziwa alifyonze hivo hivo ili kuweza kusisimua maziwa kutoka.

 Mtoto anaweza kuishi kwa maziwa ya mama tu katika moezi 6 ya mwanzo. 

Haihitajiki kumpa hata maji,  watoto hawana kiu,  maana maziwa ya mama yamejitosheleza

Kumnyonyesha mtoto ipasavyo kunaweza zuia upatikanaji wa mimba hadi kwa miaka miwili

Kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kunamjengea mtoto hali ya ukaribu na mama pia utu wema

 Pia chinibya miezi sita ya mwanzo kama mtoto atalishwa vyakula vingine bila usafi na uchaguzi sahihi,  mtoto huyu anaweza pata magonjwa ya kuhara hata utapiamlo

Ni vyema mama kuzingatia usafi wa mwili wake,  chumba,  kitanda na nguo za mtoto kuzuia magonjwa ya ngozi na mafua

Na hapa ni vyema kutumia nguo za pamba (cotton) maana nguo zingine za sufi,  nylon nk huweza sababisha upele kwa mtoto

 Pia ni vyema kumpaka mtoto mafuta ya maji kichwani ili kulainisha ngozi ya kichwa na kuzuia ukoko, Utokanao na ukavu wa ngozi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s